UBATIZO MAJI MENGI
SOMO: UBATIZO WA MAJI MENGI WA KIBIBLIA
Ni muhimu kufahamu kuwa Yohana mbatizaji alimbatiza Yesu katika maji tele (MATHAYO 3:13-17).
Yesu Kristo alibatizwa katika mto Yordani kwasababu huko kulikuwa na
maji tele. Yohana mbatizaji alikuwa akibatiza sehemu zenye maji tele ili
watu waweze kuzamishwa katika maji kama tutakavyoona maana ya ubatizo
na kwa nini kuzamisha katika maji tele. Yohana mbatizaji hakubatiza
Yordani tu, alibatiza Ainoni karibu na Salimu kwa sababu huko kulikuwa
na maji tele. YOHANA 3:23 “Yohana naye alikuwa akibatiza huko
Ainoni, karibu na Salimu, kwasababu huko kulikuwa na maji tele, watu
wakamwendea wakabatizwa”. Ubatizo lazima ufanye kwenye maji tele ya
kumtosha mtu kuzamishwa.
MAANA YA NENO KUBATIZWA AU UBATIZOLugha za asili za biblia kabla ya tafsiri mbalambali ni kiebrania na kiyunani. Agano la kala iliandikwa kwa lugha ya kiebrania na again jipya iliandikwa kwa kiyunani. Katika kuifasiri biblia kwa lugha zetu kuna baadhi ya maneno machache ambayo misamiati yake ilipoteza maana halisi iliyopo katika biblia. Kwasababu lugha zingine zunakuwa na mapungufu.
Katika biblia ya lugha ya kiebrania kuna neno “BAPTIZO” lenye maana ya UBATIZO kwa Kiswahili na kwa kiingereza BAPTIZM,
Katika biblia ya lugha ya kiyunani kuna neno “BAPTO” lenye maana ‘kuzamisha au kuchovya”.
Mifano katika biblia kuhusiana na neno” BAPTO’ kuzamisha au kuchovya.
( 1 ). Tonge la ugali linavyotowelewa katika ugali kasha linazamishwa lote. Tendo hilo la kuziswa ni kubapto “bapto” katika kiyunani (YOHANA 13:26).
( 2 ). Kuchovya ncha ya kidole. Neno kuchovya hapo (LUKA 16:24) lina katika lugha ya kiyunani ni ‘BAPTO” bapto likiwa na maana kuchovya au kuzamisha.
( 3 ) Tendo la kuchovya vazi katika damu lina maana ya kubapto “ BAPTO” katika biblia ya ya lugha ya asili kwa kiyunani.
Kwahiyo biblia inapozungumzia juu ya ubatizo inazungumzia ubatizo wa maji tele.Yohana aliwabatiza watu wa Ainoni kwasababu huko nako kulikuwa na maji tele (YOHANA 3:23). Pia tunamuona mtumishi wa Mungu Filipo na owashi wakitelemka majini ili abatizwe katika maji tele (MATENDO 8:34-39). Walitelemka majini akambatiza kasha wakapanda kutoka majini (MATENDO 8:36-39).
WATU WANAOFUNDISHA JUU YA UBATIZO WA KUNYUNYIZIA MAJI KICHWANI AU USONI NAO PIA WANA MAANDIKO.
(EZEKIELI 36:25) “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafuwenu wote, na vinyago vyenu vyote”. (HESABU 8:5-7) “Kisha Bwana akanena na Musa. Na kumwambia, watwae walawi na kuwaondoa kati ya wana wa Israeli, kasha uwatakase. Nawe utawafanyia mambo haya ili kuwatakasa, nyunyiza juu yao maji yatakasayo dhambi, nao wajinyoe kwa wembe mwili wote, kasha wazifue nguo zao na kujitakasa”. Upotofu ni rahisi kuingia kama tutayatafsiri maandiko kama tupendavyo. (2 PETRO 1:20; 2TIMOTHEO 2;15).
Maana ya maandiko hayo yanayotumiwa kimakosa kuharalisha ubatizo wa kunyunyiza maji kichwani au usoni. HESABU 19:13 “Mtuawaye yote agusaye maiti ya mtualiyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi, unajisi wake ungali juu yake bado”. Kwahiyo tunaona kuwa wakati wa agano la kale mtu aliyekuwa akiigusa maiti ya mtu aliyekufa, alihesabika kuwa amenajisika kwa kuigusa tu. Alihesabika kuwa ni mwenye dhambi (unajisi) na angeweza kulinajisi hekalu la Bwana (maskani ya Mungu). Mtu aliyenajisika alihesabika kuwa safi baada ya kunyunyiziwa kichani maji ya utakaso yaitwayo FARAKANO. (WAEBRANIA 9:10 )“kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya”.Hayo maandiko wakati wake ulishapita maana sisi tunaongozwa na agano jipya, again la rohoni, aganin la kale lilikuwa na mapungufu (WAEBRANIA 8:7-9). Dhambi au uchafu unaondolewa na damu ya Yesu kwa njia ya imani (1PETRO 1:2). Hatunyuziwi maji kichwani bali damu ya Yesu ndiyo inayonyunyizwa juu yetu na kuondoa dhambi. Tendo la kunyunyiziwa damu ya Yesu ndilo linaitwa kuzaliwa kwa roho au kuzaliwa mara ya pili (YOHANA 3:3-10). Mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu (YOHANA 3:5; 1:12). Maji yanayotajwa katika YOHANA 3:3-10 ni neno la Mungu siyo ubatizo wa maji kama walimu wengi wanavyopotosha. Neno la Mungu linamsafisha mtu kama vile maji yasafishavyo (1PETRO 1:23)
KABLA YA KUBATIZWA SHARTI MTU HUYO ATUBU DHAMBI ZAKE ZOTE KWA KUMWAMINI YESU KRISTO BAADA YA KUHUBIRIWA AU KUFUNDISHWA .
Ili mtu awe na sifa ya kubatizwa kibiblia lazima atubu dhambi zake kwanza kwa kumwamini mwanawa Mungu Yesu Kristo . (MATENDO 2:37-38) “ Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha roho mtakatifu”. MARKO 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.Mtu anabatizwa baada ya kuamini na kutubu dhambi zake zote. Kuamini maana yake ni kuacha njia zako zote za awali na kugeuka au kufanya matendo ya wokovu. MATENDO 2:41 “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu”. MATENDO 8:12-13 “ Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njeme za ufalme wa Mungu na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. Na yeye Simon mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; Akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka”. Pia katika MATENDO 8:35-38 Towashi aliamini kwanza kabla ya kubatizwa na Filipo. Mtu baada ya kujifunza Neno la Mungu na kuliamini kwa moyo wake wote na kusafishwa kwa damu ya Yesu kwa njia ya imani aweza kubatizwa (MATENDO 16:31-33; MATENDO 18;8)
UBATIZO HAUFANYWI KWA WATOTO WADOGO.
Kwa kawaida watoto wadogo wanapobatizwa huwa anakuwepo mtu mzima amempakata na kujibu maswali badala ya mtomto huyo, hii siyo sahihi kibiblia EZEKIELI 18:20 “Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa babaye, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe; haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake”. Kwa msingi huo, mtu hawezi kutubu dhambi kwa niaba ya mtu mwingine. Ni muhimu kufahamu kuwa watoto wadogo ufalme wa mbinguni ni wao hata bila kutubu dhambi (MARKO 10:13-14). Sisi sote tunazaliwa tukiwa na dhambi ya asili. Tnazaliwa kwa mfano wa Adamu na si kwa mfano wa Mungu (ZABURI 51:5; ZABURI 58:3). Pasipo sheria hakuna dhambi, dhambi inahesabiwa kwa sheria (WARUMI 4:15; WARUMI 5:12-13). Mtoto anaweza kutenda dhambi kama vila kusema uongo, kutukana, uchoyo, ugomvi, kucheza dansi (mzikiwa kidunia), kuzira n.k .Lakini sasa watoto hawahesabiwi dhambi kwa kuwa hawajui mema na mabaya. Watoto hawana uwezo wa kupambanua au kutofautisha mema na mabaya. Wanafanya bila kujua kuwa ni dhambi, ndiyo maana Yesu alisema ufalme wa mbinguni ni wao.Kabla motto kuzaliwa duniani dhambi ilikuwa imekwisha kuwako. Adanu na Eva walitenda dhambi kabla ya kuwazaa watoto wao (WAEBRANIA 5:13-14). Mwenye uwezo wa kupambanua mema na mabaya ni mtu mzima, motto mdogo akifa anaenda mbinguni moja kwa moja bila kizuizi chochote.
YESU ALIWABARIKI WATOTO HAKUWABATIZA.
Yesu mwenyewe aliwabariki watoto hakuwabatiza. Watoto wadogo wanabarikiwa tu haturuhusiwi kuwabatiza watoto wadogo. Ubatizo unafanya kwa mtu baada ya kulisikia Neno la Mungu na kutubu dhambi zake zote. Lazima mtu asafishwe dhambizake kwanza kwa damu ya Yesu kwa njia ya imani. Yesu mwenyewe alibarikiwa akiwa motto mdogo na kubatizwa akiwa mtu mzima (LUKA 2:27,34; LUKA 3:21-23).
YESU KRISTO ALIBARIKIWA AKIWA MTOTO NA KUBATIZWA AKIWA MTU MZIMA.
Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni kielelezo au mfano wa jinsi tunavyotakiwa kuishi na kutenda , alibarikiwa akiwa motto mdogo (LUKA 2:27,34). Yesu Kristo akaonesha mfano kwa kubatizwa akiwa mtu mzima na akasema ndivyo inavyotupasa kuitimiza haki yote (LUKA 3:21-23; MATHAYO 3:13-17). Tunaona Yesu alibarikiwa na mtumishi wa Mungu Simion akiwa motto mdogo, na kubatizwa akiwa na umri unaokaribia miaka thelathini. Tunapaswa kujifunza kwa Kristo (1 PETRO 2:21; 1WAKORITHO 11;1, MATENDO 2:37-41). Watu waliobatizwa wakati wa kanisa la kwanza walikuwa wengi sana hivyo walikuwa na umri wa miaka tofauti.Kigezo kinachotumika ni utu uzima, yaani uwe na uwezo wa kupambanua mema na mabaya (WAEBRANIA 5;13-14).
.UWEZEKANO WA KUBATIZWA MARA MBILI AU ZAIDI.
Wapo watu wengine watasema mimi nilishabatizwa tangu mwanzo toka utotoni, sasa itakuwaje baada ya kugundua kuwa nilibatizwa kimakosa?. Wapo watu ambao walibatizwa mara mbili katika biblia ingawa mwanzo walibatizwa katika maji tele (MATENDO 19:3-5). Ikiwa mwanzo tulibatizwa kwa ubatizo usio wa kibiblia, tunapaswa kubatizwa ubatizo wa kibiblia kama Yesu alivyosema tujifunze kwake (MATHAYO 11:29). Huhitaji kuomba ushauri kwa mtu yeyote, ni kulitii Neno la Mungu tu bila kulijadili kwanza. Ubatizo wa kibiblia unafanywa kwa mtu mara moja tu. Mtu anayetakiwa kubatiza sharti awe ni mwanafunzi wa Yesu. (YOHANA 4:2). Kama ulibatizwa bila kutubu dhambi kwanza huo sio ubatizo wa kibiblia ni sawa na mtu aliyeoga majini tu. Kama ulibatizwa utotoni unahitaji kutubu dhambi zako mwenyewe na ndipo utaweza kubatizwa kibibli. Kama ulinyunyiziwa maji kichwani au usoni hujabatizwa kibiblia. Lazima uzamishwe katika maji na ndipo unakuwa umeshiriki mauti ya Kristo (WAKOLOSAI 2:12, WARUMI 6:4-5).
TUNABATIZWA KATIKA MAJI MENGI ILI TUWE WA KRISTO.
Hatuna budi kufahamu kuwa safari Yetu ya kuelekea mbinguni inafananishwa na safari ya wana wa Israeli kuelekea Kanani (1WAKORINTHO 10;11). Mungu alimtumia Musa kuwaokoa waisraeli mikononi mwa Farao ili wamtumikie na leo hii kamtuma Mwanae wa pekee Yesu Kristo ili kutuokoa kutoka utumwani mwa Shetanui ili tumtumikie Mungu.
Ni muhimu kufahamu kuwa ubatizo ulikuwepo tangu zamani za agano la kale. Waisraeli walibatizwa ili wawe wa Musa (1WAKORINTHO 1O:1-2). Tunabatizwa sawasawa na agizo la Yesu ili nasi tuwe wa Kristo. Ni muhimu kufahamu kuwa kuzamisha katika maji tele kibiblia ni sawa na kuzikwa ndiyo maana ubatizo ni mara moja tu. Tunazikwa na kufufuka na Kristo kwa njia ya ubatizo. Hapa ndipo tunashiriki mauti ya Kristo (WAKOLOSAI 2:12). Utii wa kwanza kwa mtu baada ya kuokoka ni kukubalikuzikwa na kufufuka pamoja na Kristo (WARUMI 6:4-5). Kwahiyo kubatizwa katika maji mengi kunatufanya kushiriki mauti ya Kristo yaani kuzikwa na kufufuka kwake. Maji yanakuwa kama kaburi tu ambayo mtu anazamishwa ndani yake ili kushiriki mauti ya Yesu kibiblia (WAKILOSAI 2:12, WARUMI 6:4-5).
KUWA TAYARI KUTIMIZA HAKI YOTE.
(MATHAYO 3:13-15)
Yesu Kristo alisema “ndivyo inavyotupasa kutimiza haki yote”.Kutimiza haki yote maana yake nini? Tunaona maana ya haki yote katika (ZABURI 119:172) . Haki yote ni maagizo yote (ZABURI 119:6). Tunapaswa kutimiza haki yote (maagizo yote ) ya Yesu. Yesu Kristo alitimiza haki yote ingawa alikuwa hana dhambi na ndiyo maana Yohana mbatizaji alishangaa na hakutaka kumbatiza akisema kuwa yeye hastahili kabisa kumbatiza. Tunatakiwa kuwa tayari kutimiza haki yote kama Yesu alivyofanya. Wana wa Israeli walibatizwa mara tu walipotoka katika utumwa wa Farao na sisi tunapaswa kubatizwa mara tu tunapotoka katika utumwa wa dhambi au utumwa wa Shetani.
- Je, wanafunzi wa yesu walibatizwa?
- Je, paulo mtume alibatizwa katika maji tele?
18 |
And straightway there fell from his eyes as it were scales, and he received his sight; and he arose and was baptized; |
- Je. Askari wa gereza na watu wa nyumbani mwake walibatizwa katika maji tele?
(MATENDO 16:30-34).
Agizo
la Yesu kwa wanafunzi wake kwa kila aaminiye kuwa ni sharti abatizwe,
wanafunzi wake hawa walilitendea kazi. Tunaoan kuwa walibatizwa lakini
kuna watu ambao siku hizi ambao hutafuta andiko la kupindisha ukweli
ili kuharalisha uovu wao Bila shaka watumishi hawa waliwapeleka mahali penye maji mengi na kuwabatiza kwa kuwazamisha ili washiriki mauti ya Yesu kuzikwa na kufufuka kwake (WAKOLOSAI 2:12; WARUMI 6:4-5).
- Kama mtu yupo mahali ambapo hapana maji mengi kama jangwani atabatizwa wapi?
Kwa Mungu hakuna udhuru wowote, yeye akiagiza haunabudi kulitendea kazi agizo hilo. Kwa gharama yoyote tunapaswa kuhakikisha tunatimiza haki yote kwa kubatizwa katika maji tele., Hatuna budi kusafiri kuyafuata maji yaliko kwa gharama yoyote. Kama Malkia wa Kushi aliweza kusafiri umbali mkubwa kwenda kuitazama hekina ya Sulemani Yesu anasema huyo atawahukumu watu wenye udhuru wa umbali. Wanadamu wanatafuta visingizio ili wasibatizwe katika maji tele kibiblia.
- Je, ikiwa nilibatizwa kwa kufuata mkumbo nifanye nini?
- Je, ikiwa nilibatizwa na mtu ambaye hakubatizwa katika maji tele nifanye nini?
- Je, ikiwa nilibatizwa na mtu ambaye haamini ubatizo wa maji tele nifanye nini?
- Je, kama mtu alibatizwa kibiblia hatimaye akarudi nyuma kiroho, akitubu atabatizwa tena?
- Je, tunabatiza kwa jina la nani?
Ubatizo wa kibiblia unafanya kwa mtu mara moja tu. Tena tunabatiza kwa jina la Baba,na Mwana, na Roho mtakatifu. Tunachovya au kuzamisha mara moja tu na si mara tatu kama majina yalivyo. Tunazamisha mara moja kama Yesu alivyozikwa mara moja.
- Je, mbona mitume wa yesu walibatiza kwa jina la yesu?
Kielelezo chetu siyo mitume bali ni Kristo. Paulo anasema tumfuate yeye kama anavyomfuata Kristo (1 WAKORINTHO 11:1). Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake, wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka (YOHANA 13;16). “Kwa jina la” ina maana “kwa ajizo la”. (ESTA 8:7-10). Hii ilikuwa inatumika hivyo wakati wa bablia lakini siku hizi ni tofauti na hapo zamani. (ESTA 13:16). Kwa jina la mfalme yaani kwa agizo la mfalme. (ESTA 13:10). Walitaka kutofautisha ubatizo uliofanyika kwa jina la (agizo la ) Yohana na ubatizo wa jina la (agizo la ) Yesu. ( MATHAYO 3:4-6; 3:1-3). Kutokana na kwamba watu wengi walikuwa wameshabatizwa ubatizo wa Yohana, ndiyo maana mitume wakawabatiza tena kwa jina la (agizo la) Yesu. Yesu ni mkuu kuliko Yohana. Mitume walibatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu., kama lilivyo agizo lake Bwana wetu Yesu Kristo..Mungu akikuagiza jambo la kufanya, usipunguze wala usiongeze lolote au kusahihisha (KUMBUKUMBU 12:32). Kwahiyo, tumeagizwa kubatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu (MATHAYO 28:19).
- Je, kama mtu amebatizwa kwa roho, anaweza kubatizwa kwa maji tena? (MATENDO 10:44-46).
- Je ubatizo wa nyumba yote unapotajwa katika biblia si pamoja na watoto wadogo?
( MATENDO 18:8; 16:31-33 )
Katika tamaduni za wakati wa biblia, watoto hawakuruhusiwa kuwepo eneo
lenye watu wazima ndiyo maana wanafunzi wake Yesu walitaka kuwafukuza ( KUMBUKUMBU LA TORATI 3:5-6 ). Hata katika hesabu za watu watoto hawakuhusishwa katika hesabu ( 1 SAMWELI 22:19; EZRA 10:1; YEREMIA 40:7 ). Watoto hawakubatizwa katika familia zao ( 1 WAKORINTHO 1:10-11; MATENDO 10:1-2 ). Mtoto mdogo hawezi kumcha Mungu, hivyo biblia inaposema nyumba nzima ikabatizwa ina maanisha watu wazima.- Kubatizwa na kutokubatizwa ni sawa yaani hakuna umuhimu wowote wa kutahiriwa.
- Mbona maandiko yanasema tusiweke msingi tena wa mabatizo.
- Je mtu anapobatizwa ni lazima kubadilisha jina?
- Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanywaje?
- Je mtu asipobatizwa kwa maji mengi hawezi kuingia mbinguni? Kama ndiyo mbona yule mnyanganyi aliingia?
- Nikiamua kubatizwa kinyume na mafundisho au maagizo ya wazazi wangi si watanilaani.
Mungu anataka tuzishike amri zake, tusizishike amri za wazazi pale zinapokuwa kinyume na Mungu. ( HESABU 23;8; MITHALI 26:2 ).
- Je kama katika dhehebu letu tunafundishwa kuwa ubatizo tunaobatizwa umepitishwa katika vikao vyao kama Mungu alivyosema ‘ lolote mtakalolifunga duniani na mbinguni litafungwa na litakalofunguliwa duniani pia mbinguni litafunguliwa”.
TUBUNI MKABATIZE SAWASAWA NA AGIZO LA YESU
MATENDO YA MITUME 2:38
Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!
Comments
Post a Comment